The perfect plan for booklovers!
Add this book to bookshelf
Grey
Write a new comment Default profile 50px
Grey
Subscribe to read the full book or read the first pages for free!
All characters reduced
sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu - cover

sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu

Alain Mabanckou, deborah ellis, Paul Theroux, Mahmood Mamdani, Ngũgĩ wa Thiong’o, alexandra fuller, William Kamkwamba, Jack Mapanje, RICHARD MABALA, EMANUEL MBOGO, OXFORD TANZANIA, OXFORD KENYA, ERIC SHIGONGO, ABRAHAM R. MENGI, BENJAMIN W. MKAPA, JULIUS K. NYERERE, PRO. ISSA SHIVJI, shaaban robert, shafi adam shafi, peter palangyo, agoro anduru, prince kagwema, elvis musiba, jean de dieu musabyimana, clementine wamariya, alexis kagame, jeanne habyarimana, okello oculi, yoweri museveni, okot p'bitek, laban lo liyong, Tansi Sony Labou, emmanuel dongala, fransisco santos, agostinho neto

Publisher: SAMSON JOSEPHAT MANYALA

  • 0
  • 0
  • 0

Summary

Kim Ung-yong alizaliwa nchini Korea ya Kusini katika jiji la Seoul. Alipokuwa na umri wa mwaka mmoja tu, tayari alikuwa amejifunza alphabeti za Kikorea na alphabeti 1,000 za lugha ya Kichina. Alipofikisha umri wa miaka mitatu alikuwa anaweza kufanya hisabati ngumu za mada ya 'calculus'. Kim alipofikisha umri wa miaka mitano, tayari alikuwa ametunga, kuchapisha na kuuza kitabu chake cha kwanza. Ni katika umri huo wa miaka mitano Kim alikuwa akiongea vizuri lugha za Kikorea, Kijapani, kingereza, Kifaransa na Kijerumani! Kitabu hiki kimesheheni mifano ya watoto waliozaliwa na akili za juu kama Kim. Hawa ni watoto ambao kila mzazi angetamani kuwanao. Ni kweli kwamba, sababu za vinasaba 'genetic' zaweza kuwa moja ya vyanzo vya mtoto kuzaliwa na akili za juu kuliko kawaida (more than 100% of IQ), lakini tafiti za kisayansi zinamletea mzazi kanuni nyepesi za kumwezesha kumzaa mtoto mwerevu. Kanuni hizo, ndizo mada zilizomo kitabu hiki.

SAYANSI YA KUMZAA MTOTO MWEREVU  ni kitabu kinachomfundisha mzazi namna ya kumzaa (kumpata) mtoto ambaye kama hatafikia kiwango cha kuitwa "prodigy" au "genius", basi ataitwa mwerevu; yaani binadamu mwenye uwezo mzuri katika kuyamudu masomo yake na kutatua changamoto za maisha. Elimu hii, inamuandaa mtoto kuanzia mazingira ya kabla ya kutungwa kwa mimba yake; kichanga tumboni; kuzaliwa na kufikisha umri wa miaka minne.

Mtoto aliyeandaliwa kwa sayansi hii, daima atakuwa ni mshindi masomoni na maishani. Kitabu hiki, ni mkusanyiko wa tafiti zilizofanywa na wataalamu mahiri wa mambo ya afya, saikolojia, elimu, sanaa na wengineo katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Ulaya, Asia na Australia. Baadhi ya tafiti hizi zimechukua takriban muda wa miaka 40 ili kukamilika!

Msomaji atagundua kwamba, kabla hajafanya uamuzi wa kuzaa na mwenza wa namna gani, alipaswa kwanza kupata maarifa yaliyoko humu. Lakini pia, kama tayari uchaguzi wake haukuwa wa kisayansi katika kumchagua mwenza, basi bado yapo maarifa ya kurekebisha dosari za kumzuia kumpata mtoto mwerevu. Kitabu bado chafaa kabla ya ujauzito, na kama mzazi amechelewa kupata maarifa haya, basi elimu hii bado itafaa endapo mtoto hajafikisha umri wa miaka minne. Hilo ni angalizo muhimu lenye sababu za kibaiolojia.

Bi. Janeth Kalinga ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DUCE), pamoja na mwandishi mahiri wa vitabu Mwl. Samson Manyala, wamekuandalia kitabu hiki katika lugha rahisi kueleweka. Aidha, japo mtoto na mzazi aliyeongelewa ni wakitanzania, lakini kitabu bado kinabakia kuwa ufumbuzi kwa wazazi wote wanoelewa au kutumia lugha ya Kiswahili kokote ulimwenguni. Kama ilivyo kwa Tanzania, kitabu hiki ni muhafaka vilevile kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, na Malawi. Nchi hizi, licha ya kuwa watumiaji au waelewa wa Kiswahili, lakini mazingira yao na changamoto zao kijamii, kielimu na kiuchumi hazitofautiani sana na za Tanzania.